ELIURD MWAITELEKE ATOA BENDERA ZA CCM RUNGWE

KATIKA uimarishaji wa vyama vya siasa nchini, Mdau wa Maendeleo nchini Ndugu Eliurd Mwaiteleke amekabidhi bendera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Makatibu Kata wa Kata ya Iponjola, Kiwira pamoja na kwa Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Ikuti Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.

Viongozi hao wamepokea bendara hizo leo Tarehe 16.09.2024.

Vitendea kazi hivyo vimekabidhiwa na Robert Mwandi kwa niaba ya Eliurd Mwaiteleke ambaye amesema Bendera hizo ni Moja ya vitendea kazi vya chama hicho kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Viongozi hao wamemshukuru Ndugu Eliurd Mwaiteleke na wamemuomba aendelee kuwaunga Mkono katika Uchaguzi serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani 2025.

Post a Comment

0 Comments