Na Gordon Kalulunga, Kyela
MJUMBE wa Baraza la Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya (UWT) Bi. Sarah Mwangasa amewahimiza wanawake nchini kote kujitokeza kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu 2024 na kupiga kura kuwachagua viongozi wenye sifa.
Ametoa rai Wilayani Kyela Mkoani Mbeya mwishoni mwa Juma lililopita.
Bi. Sarah amesema Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan amekuwa kielelezo cha ushupavu wa uongozi kwa mwanamke, hivyo wanawake wanayo fursa sasa ya kujitokeza kwa ajili ya kuungana na Rais Samia katika kuiletea Maendeleo jamii ya Watanzania.
"Rais Samia amekuwa kielelezo cha ushupavu wa uongozi wa Mwanamke nchini hivyo natoa shime kwa wanawake na vijana kujitokeza katika kujiandikisha na kuwania uongozi katika Serikali za mitaa mwaka huu 2024 na zaidi tuunge mkono 4R za kustahimiliana kama falsafa ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyo" alisema kiongozi huyo.
Sanjali na hayo amesema changamoto nyingi za jamii zinamgusa Mwanamke huku akizitaja baadhi ikiwemo Maji, malezi na ukatili wa Kijinsia.
0 Comments