Na Gordon Kalulunga Mwaipungu
MACHO na masikio ya wengi ni kufuatilia na kuona uandikishaji katika daftari la wapiga kura la Wakazi wa Mtaa au Kitongoji.
Ni kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa hapo Novemba 27,2024.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC Mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri (ASAS), amejitokeza na kujiandikisha KATIKA Kituo cha Afya cha PHC, Mtaa wa Saba Saba Manispaa ya Iringa.
M-NEC ASAS mara baada ya kujiandikisha alizungumza na waandishi wa habari huku akihimiza wananchi wa Mkoa wa Iringa kujitokeza kujiandikisha ili kupata haki zao za kuwapigia kura wagombea wanaowahitaji.
Aidha alisema kuwa anayo imani kuwa chama chake yaani (CCM) kinaweza kuibuka na ushindi mkubwa katika Mkoa wa Iringa na nchi nzima kwa Jumla kwa kile alichosema kuwa ni kutokana na Utekelezwaji mkubwa wa miradi ya Maendeleo.
Ndiyo maana ninasema kuwa, M-NEC ASAS amekibidhaisha chama chake kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa hapo Novemba 27, Mwaka huu.
0765615858

0 Comments