NAIBU Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amelielekeza shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhakikisha linatangaza, na kutoa elimu Kwa jamii juu ya huduma zinazotolewa na Shirika hilo.
Ameyasema hayo leo12 Oktoba ,2024 alipo tembelea makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea shirika hilo lengo likiwa ni kujua jinsi linavyo fanya shughuli zake.
" Nawaelekeza TTCL , Huduma kama simu za mezani , T-pesa ziendelee kuboreshwa, pamoja na maeneo yote ya muhimu mtandao usisumbue mfano maeneo hayo ni pamoja na kwenye mifumo ya malipo ya Serikali, katika station zote za SGR na mengine."
Hata hivyo Mhandisi Mahundi pia amelipongeza shirika la TTCL kwa huduma nzuri ya fiber mlangoni. Na ameliomba Shirika hilo kuongeza ubunifu katika huduma hii,Ili waweze kwenda sambamba na Taasisi zingine zinazo toa huduma kama hii.




0 Comments