MASACHE AWA MWAROBAINI KIJIJI CHA SHOGA

NI OCTOBER 3,2024

Mbunge Jimbo la Lupa-Chunya Mkoani Mbeya Mh.Masache N, Kasaka amefanya ziara katika kijiji cha Shoga na Igundu vilivyopo kata ya Sangambi akiwa ameambatana na diwani Mh.Junjulu N. Mhewa, Diwani(V/M) Mh.Saraphina Hongori na wajumbe wa K/Siasa Wilaya wakiongozwa na Katibu wa Chama Wilaya Comrade Jockery Selemani aliweza kutembelea ujenzi wa mradi wa maji ulio chini ya RUWASA.

Sambamba na hilo Mbunge Masache alisikiliza kero za wananchi na kuzipatia Majibu. 

Pia alielezea Miradi iliyofanyika kata ya sangambi, hasa kijiji cha Shoga ikiwepo Barabara, Madarasa, Umeme pamoja na Maji. 

Mhe. Masache amemshukuru Mhe. Rais Samia na serikali kwa kuendelea kuleta Fedha za miradi mbalimbali, pia amempogeza diwani Mh. Junjulu kwa usimamizi mzuri wa miradi katika Kata hiyo.

SAMIA NA MASACHE

CHUNYA KAZI INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments