2819 WAHITIMU CHUO KIKUU CUOM MBEYA MAHAFALI YA 10 MGENI RASMI MH MAHUNDI

 


JUMLA ya wahitimi 2819 wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mbeya wamehitimu katika kada mbalimbali ikiwa ni mahafali ya 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho huku mgeni rasmi akiwa ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii Jinsia Wanawake na makundi Maalumu ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi  Maryprisca Mahundi.

Katika mahafari hayo Wanaume waliohitimu ni  1376 na Wanawake ni 1443 ambapo wanachuo 686 wameshindwa kumaliza masomo yao kutokana na sababu mbalimbali.

Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Romward Haule amesema Chuo kimekuwa kikipokea maombi mengi kutokana na ubora wa wakufunzi,vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Akitoa taarifa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha CUoM Godfrey Mwasekaga amewataka wahitimu wajiajiri badala ya kutegemea ajira sanjari na kuiomba Serikali iweze kuwasaidia watu wenye kipato cha chini.

Katika hotuba yake Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii Jinsia Wanawake na makundi Maalumu Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapongeza wazazi,walezi na wafadhili kwa kufanikisha wahitimu kumaliza masomo yao.

Aidha amewataka wahitimu kutumia elimu yao kuisaidia jamii na kwa kutambua hilo Serikali imeendelea kuongeza fedha nyingi kwa ajili mikopo na itaendelea kuongeza fedha ili kuendelea kusomesha idadi ya wanachuo.

Hivi sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa elimu ngazi ya vyuo kutokana na Serikali kuongeza mikopo ya elimu huku ikiendelea kutoa elimu zaidi ya kujitegemea ili wahitimu wajiajiri badala ya kutegemea ajira.

Post a Comment

0 Comments