Pamoja na salamu za kuwatakia kheri ya Mwaka Mpya 2026. Napenda kutumia nafasi hii , kumshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyemwingi wa huruma, kwa neema yake juu ya maisha yetu.
Tumepitia mengi tangu tuianze Jumapili ya kwanza mwezi Januari hadi leo hii tunaifikia Jumapili ya mwisho katika mwaka huu.
Yapo mengi mema Mungu ametufanyia, yapo mengi magumu adui alitupitisha, mengine magumu Mungu aliruhusu yatupate ili tuimarike zaidi imani zetu kwa kuutafuta msaada na uso wake hasa pale tulipotaka kukengeuka maana anatupenda.
Iko mishale mingi ilielekezwa kwetu lakini katika yote Bwana amekuwa ngome na ngao yetu, mlinzi, mwamba na mtetezi wetu, amekuwa jabali letu na kinga yetu. Hakutuacha tufanywe mateka kwa adui zetu, hata pale walipotaka kula nyama zetu, hakutuacha tuwe mawindo yao wabaya wetu. Kuishi kwetu hata leo ni kwasababu ya neema yake. Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi nafsi yangu na iseme sasa!
Katika hayo yote jua lipo kusudi Mungu anataka tulitimize, hivyo kabla hatujaingia 2026 tumuulize Mungu anataka tusimame wapi ili tukitimiza kwa msimu mwingine ujao.
Happy Last Sunday of the year 2025, in advance. Na tunapoukaribisha Mwaka Mpya . Namuomba sana Mungu akaguse hitaji la moyo wako na Mwaka mpya ukawe wa tofauti kwako, Mungu akakupandishe viwango tofauti ili wakati ukifika , uje utoe ushuhuda wako kwamba katika hili namshukuru Mungu.
Ndugu zangu , Kwa pamoja tudumishe amani, umoja , mshikamano, undugu na upendo katika kuijenga Nchi yetu Tanzania . Neema ya Mungu ipitayo vitu vyote ikawe juu yako. Amen .
Happy New 2026 Year.
Paul Douglas Mwakajumba
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa


0 Comments