Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu Eng. Maryprisca Mahundi amewataka vijana kusimama kusimama imara kukemea Uchochezi na upotoshwaji unaoenezwa mitandaoni dhidi ya Serikali na kusimama imara kuitetea Serikali kwa hoja zenye nguvu.
Eng.Mahundi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vijana wa UVCCM Tawi la Chuo Cha ADEM Kampusi ya Mbeya katika mkutano maalumu wa Tawi la UVCCM chuoni hapo.
"Tujitokeze kukemea Uchochezi dhidi ya serikali yetu unaoenezwa mitandaoni,tueleze mazuri ya serikali yetu kwa hoja" alisema Eng Mahundi.
Aidha Naibu Waziri Mahundi ambaye pia ni Mbunge Viti Maalumu anayewakilisha Wanawake UWT Mkoa wa Mbeya kuwa mstari wa mbele kulinda amani na utulivu wa nchi jambo ambalo litachangia kuwa na fursa ya kufanya shughuli za kujiongezea kipato na kujiinua kiuchumi.
Amesema Vijana wanapaswa kutumia vyema nguvu na Elimu yao kwa kujiendeleza kiuchumi kwa kuwa Maendeleo ya nchi yanategemea zaidi Elimu na nguvu walizonazo.





0 Comments